The House of Favourite Newspapers

MWANZA: MPWA WA SHIGONGO AUVUA UKAPELA

Mama mzazi wa Edna Manyilizu ambaye ni mfanyakazi wa Global (kushoto) akifuatilia kilichokuwa kikiendelea kanisani.
Mama wa Emmanuel Aron aitwaye Tabitha (mwenye mkoba) akipita mbele kuwapongeza wanaye.
Bwana harusi, Emmanuel Aron akimvisha pete mkewe, Christina John.
…Christina John akimvish pete mmewe.
Sehemu ya ndugu wa bwana harusi walipokaa wakati wa ibada kanisani.
Dada wa bwana harusi aitwaye, Asteria Aron (mwenye mtoto) akiwa kanisani hapo.
Kaka zake bwana harusi wakiongozwa na James M. Bukumbi wakipita mbele kumpongeza ndugu yao.
Bwana harusi na bibi harusi wakila kiapo mbele ya padri.

 

MPWA Wa Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group Ltd aitwaye, Emmanuel Aron, wa Jijini Mwanza leo amefunga pingu za maisha na mrembo, Christina John.

 

Ndoa hiyo imefungwa katika kanisa la Familia Takatifu Nundu-lililopo Meco Jijini Mwanza  huku ibada ya harusi hiyo ikiongozwa na Padri Moses Mapera.

 

Katika mahubiri yake Padri amewaasa wanandoa hao kuwa watu wenye kuheshimiana, kuombeana msamaha pale wanapokesea ili waweze kufurahia ndoa yao.

 

Alisema kuwa kama wanandoa hao wataheshimu misingi yote ya harusi ikiwemo upendo na mambo mengine ndoa hiyo itakuwa imara milele na milele.

 

Amewataka wanandoa hao kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo ili familia hiyo iweze furahia maisha kama mungu anavyopendezwa.

 

Comments are closed.