The House of Favourite Newspapers

Mwenyekiti Chama cha Ushirika Pwani (CORECU) Atangaza Neema Kwa Wakulima

0
Mwenyekiti wa CORECU, Mussa Mng’aresa akizungumza na Global Tv, Kibiti Pwani.

 

 

MWENYEKITI wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoa wa Pwani kinachoshughulika na zao la ufuta na korosho (CORECU), Mussa Mng’aresa amewaondoa shaka na kuwarudisha kundini wakulima wa mkoani humo waliokuwa wamekwazika na kuyasusa mazao ya ufuta na korosho.

Wakulima hao walikwazika na changamoto mbalimbali na kuamua kuikata mikorosho na kufyeka ufuta ili wapande mazao ya chakula kutokana na changamoto walizokuwa wakikumbana nazo.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge.

 

 

Akizungumza na Waandishi wetu Mng’aresa amesema hapo awali wakulima walikuwa na malalamiko mengi sana kufikia wengi wao kuazimia kujiondoa kwenye Chama Kikuu cha Ushirika (CORECU) lakini serikali iliposikia kilio chao ilivunja bodi iliyokuwepo na kuunda bodi ya mpito ya mwaka mmoja kwaajili ya kufuatilia kero zilizokuwa zikiwakwaza wakulima hao.

Mng’aresa aliendelea kusema;

Mwenyekiti wa CORECO Mussa Mng’aresa akizungumza na mwandishi wetu Issa Mnally.

 

 

“Namshukuru Mungu katika bodi hiyo ya mpito mimi ndiye niliyekuwa mwenyekiti nikiwa na wajumbe wenzangu 6, kutoka kila wilaya ambapo mpaka sasa tumeshazimaliza changamoto karibu zote zilizokuwa zikiwakwaza wakulima. “Tatizo la kwanza lililokuwa likiwakwaza wakulima hao ni ucheleweshewaji wa malipo yao.

Mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Khadija Nasri.

 

 

“Malipo yalikuwa yakichelewa sana lakini sasa hivi tumeshatoa maagizo kwa mnunuzi yeyote anayeshinda mnada wa ununuzi, ndani ya siku mbili awe ameshawalipa wakulima na ndani ya siku 4 awe ameshachukua mizigo yake”. Amesema Mng’aresa.

Zao la ufuta.

 

Mwenyekiti huyo aliendelea kusema;

“Kero nyingine iliyokuwa ikiwakwaza wakulima ni kupunjwa fedha zao kwenye vyama vya msingi, kwakushirikiana na serikali ya wilaya na mkoa wametoa sapoti kubwa sana kwa kuwadhibiti waliokuwa wakifanya uhuni huo na sasa kero hiyo imepungua kwa asilimia 80% na bado tunawafuatilia wanunuzi wasio waaminifu ili kulimaliza kabisa tatizo hilo.

Zao la korosho.

 

“Mpaka sasa bado kuna vyama vya msingi bado vinaendelea kuwababaisha wakulima lakini ole wake tutakayembaini.

“Nimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani, na wakuu wa wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji kwa kuwaweka ndani viongozi walijaribu kuwaletea ubabaishaji wakulima kwenye malipo ya mazao yao.

“Hivyo nawaomba wakulima waondoe hofu wasahau yaliyopita wasiwe na wasiwasi tena sasa ni wakati wa wazee kwa vijana tuingie mashambani kwa maana sasa hivi uchumi upo mashambani hiki siyo kipindi cha kulalamikia tatizo la ajira kwani kilimo kwa sasa kupitia CORECU ni ajira tosha kabisa.

“Hapo awali wakulima walikuwa wakiuza ufuta shingi 800 mpaka 1,200 lakini sasa tumeboresha maslahi ya wakulima ambapo wanauza kwa shilingi 3,020 kwa kilo bei ambayo imepanda mno kwaajili ya kumnufaisha mkulima.

“Nitumie nafasi hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye ameshatoa dira kwa kutoa ruzuku ya mbegu, pembejeo na vitu vingine kwaajili ya wakulima hivyo tuitumie hiyo fursa kama ajira”.

Mng’aresa alitoa namba yake ya simu namba 0715310779 kwa mkulima yeyote mkoani Pwani atakayekumbana na changamoto yeyote haswa kutoka katika vyama vya msingi.

 

Mng’aresa alitumia nafasi hiyo kumshukuru Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga kwa kushughulikia tatizo la barabara ya kuingia na kutoka katika Kata ya Kisegese ambayo inalima sana zao la ufuta lakini ilikuwa na tatizo la barabara lakini alipomfikishia kilio hicho kutoka kwa wakulima mara moja ameanza kuighulikia barabara hiyo ambapo mpaka sasa matengenezo ya barabara hiyo yanaendelea.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY /PWANI  

Leave A Reply