The House of Favourite Newspapers

Mwenyekiti Wa Nacopha Awafunda Vijana

0

Mwenyekiti wa baraza la watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (Nacopha) Bi. Leticia Mourice,amewafunda vijana waliohudhuria katika mdahalo wa kitaifa wa viongozi wa dini na vijana,uliofanyika leo katika ukumbi wa Tugimbe, jijini Mbeya,ambapo aliwahasa vijana,kuacha kufanya ngono zembe,na kusisitiza kuwa wote wanatambua kufanya mapenzi ni haki ya msingi ila inategemea ni wakati gani, wapi na ni nani unafanya naye mapenzi.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa pia vijana wakiume waache kabisa kujiingiza kwenye tamaa,za kupenda watu wazima kwasababu tu ya kupenda kupewa vitu vya bure na matokeo yake kuibuka na maradhi kwaajili tu ya kufanya ngono zembe.

Kwa upande wa viongozi wa dini,Mchungaji wa kanisa Pentekoste, Erica Mwakyokile,amesema kuwa anasikitika sana na baadhi ya viongozi wa dini ambao,wanashindwa kufanya huduma ipasavyo,badala yake wanamrubuni mgonjwa ambaye anatumia dawa za kurefu maisha za ARVs, aache kwasababu atakuwa ameshapona kupitia uponyaji wa kanisa husika,kitu ambacho sio sahihi kabisa,kwasababu hakuna uthibitisho wowote kutoka kwa madaktari na wataalamu wa masuala ya VVU na Ukimwi.

Mchungaji huyo alisisitiza kuwa viongozi hao wa Dini nchini wametakiwa kutumia majukwaa yao katika kusaidia Mapambano dhidi ya Virusi Vya UKIMWI ikiwamo kutoa elimu sahihi badala ya kushawishi Waviu kuacha dawa.

Ambapo kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Dk. Vicent Anney, wakati akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Juma Homera kwenye Mdahalo wa Viongozi wa Dini na Vijana kuhusu UKIMWI, amesema Viongozi hao kwa wakati mwingine wamekuwa ni sababu ya watu wanaoishi na VVU kuacha kutumia dawa kwa kuamia kuwa wanaweza kupona kanisani.

“Viongozi wa Dini ni watu mnaoaminiwa sana na Jamii, hivyo hamna budi kutumia majukwaa yenu ya dini kwa ajili ya kutoa Elimu sahihi ya UKIMWI badala ya kuwaeleza waumini kuwa wanaweza kupona kwa maombi.

“Kwani hakuna mahala kwenye Biblia au Msaafu ambapo pame andikwa kuwa kutumia dawa ni dhambi, hivyo tumieni vituo vyenu vya Televisheni mtandao kwa ajili ya kujenga mtazamo chanya wa matumizi ya dawa za ARVs kwa Waviu na si kuwambia waache dawa,” amesema Dk. Anney.

 

Ameongeza kuwa kama ambavyo Viongozi wa Dini hawakatazi waumini wao kutumia dawa za Malaria basi wanapaswa kufanya hivyo pia kwenye ARVs na Chanjo ya Uviko- 19.

 

Mdahalo huo ulioandaliwa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) unaoendelea ukihusisha Viongozi wa Dini na Vijana ambao ni sehemu ya Maadhimisho ya UKIMWI duniani ambayo Kitaifa yatafanyika jijini Mbeya Desemba Mosi yakiwa na Kauli mbiu ya “Zingatia Usawa, Tokomeza UKIMWI, Tokomeza Magonjwa ya Mlipuko”.

 

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, yatakayiifanyika katika viwanja vya Ruandanzovwe.

 

Awali, akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko, alisema lengo la mdahalo huo ni kujadili mchango wa Viongozi wa Dini katika mwitikio wa VVU na UKIMWI nchini.

HABARI NA IMELDA MTEMA | GPL

Leave A Reply