The House of Favourite Newspapers

MWIGULU AKABIDHI OFISI KWA LUGOLA – PICHAZ

ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba amemkabidhi ofisi Waziri Mpya wa Wizara hiyo, Kangi Lugola katika Makao Makuu ya nchi Jijiji Dodoma leo Jumanne, Julai 10, 2018.

 

Kupitia ukurasa wake wa Twiter, Mwigulu ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi ameandika; “Makabidhiano ya ofisi/kijiti hii leo Dodoma. Nimemtakia kila raheli Mh.Kangi Lugola katika utumishi wake kwa watanzania katika wizara hii.

 

Aidha Mwigulu Nchemba mara baada ya kuenguliwa nafasi hiyo alifika jimboni kwake na kuongea na wanachi wake akisema kuwa sasa atapa nafasi ya kuwatumikia vyema wananchi wake.

Julai 1, 2018 Rais John Pombe Magufuli alifanya mabadiliko ya Balaza lake la Mawaziri na kumteua Mbunge wa Mwibara na aliyekuwa Naibu Waziri wa Muungano na Mazingura, Kangi Lugola kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi akichukua nafasi ya Mwiguku.

Comments are closed.