The House of Favourite Newspapers

Mwigulu: Hatuwezi Kuacha Kukopa Kuogopa Deni Kuwa Kubwa ni Kwa Ajili ya Maendeleo

0
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba.

 

Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema haiwezekani kuacha kukopa kwa kuogopa deni kuwa kubwa, mikopo ya Serikali ni kwa ajili ya Maendeleo ya Miradi mikubwa ya Nchi na siyo ya kulipia Mishahara au Matumizi ya kawaida.

 

Amesema Deni la Serikali kwa sasa uwiano wake na Pato la Taifa ni 31% wakati ukomo ni 55%, Deni la Nje kwa Uwiano wa Pato la Taifa ni 18% wakati ukomo wake ni 40%, Deni la Nje kwa mauziano ya nje ni 142% ukomo ni 180%

 

Waziri ameongeza “Tunafurahia 4G na 5G lakini Mkongo wetu wa Taifa ni deni, miradi ya aina hiyo ni mingi. Mradi ukishakopewa hauwezi kusimama, fedha zinapoingia ndivyo deni linavyokua. Mfano kuna madeni nimesaini yalipwe ambayo yalikopwa kabla sijazaliwa”

Leave A Reply