The House of Favourite Newspapers

MWIJAGE: Taarifa Rasmi ya Serikali Kuhusu Mafuta ya Kula- Video

Waziri mwenye dhamana ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, amewasilisha Bungeni ripoti juu ya sakata la upungufu wa mafuta ya kupikia nchini pamoja na meli zenye mafuta zilizokwama bandarini kutokana na ushuru.

Ripoti hiyo ya Waziri Mwijage imetokana na agizo alilopewa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, la kumtaka kutoa maelezo ya kina juu ya suala hilo ambapo waziri amesema ni asilimia 30 tu ya mafuta ndiyo yanazalishwa nchini huku asilimia 70 yakiwa ni mafuta ya kutoka nje ya nchi.

 

Mwijage ameanisha namna ambavyo TBS hupima mafuta hayo kubaini kama ni crude oil (ghafi) au ni safi ambapo kipimo cha kwanza ni Fee Fatty Acid (FFA) na cha pili ni rangi ya mafuta hayo.

MSIKIE MWIJAGE AKITOA RIPOTI HIYO BUNGENI

Comments are closed.