The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Makongoro Wawasili Kijijini Marasibora Tarime, Kuzikwa leo

0

Makongoro1Mama wa marehemu, Makongoro Oging’, Bi. Magreth Oging’ akilia kwa uchungu mara baada ya mwili wa mwanaye kuwasili nyumbani.Makongoro5Jeneza lenye mwili wa marehemu Makongoro likiingizwa ndani.Makongoro2Kiongozi wa kijiji akipuliza pembe kama njia ya jadi ya mawasiliano kuwajulisha waombolezaji wengine kuwa tayari mwili wa marehemu Makongoro umewasili nyumbani hapo.Makongoro3Ndugu, jamaa na marafiki wakipokea mwili wa marehemu.Makongoro4Mmoja wa ndugu wa marehemu Makongoro akiwa amezimia.

MWILI wa aliyekuwa Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Makongoro Oging’ umewasili nyumbani kwao Kijiji cha Marasibora wilayani Tarime mkoani Mara saa nne usiku jana ambapo leo shughuli ya mazishi inatarajiwa kufanyika.

Makongoro Oging’ aliaga dunia Mei 21 jijini Dar es Salaam na kuagwa juzi Mei 26 katika hospitali ya Amana Ilala ambapo siku hiyo hiyo mchana, safari ya kuusafirisha mwili wake kuelekea kijijini kwao Marasibora Tarime ilianza. Mazishi ya Makongoro yatafanyika leo nyumbani kwao Marasibora.

PICHA NA RICHARD BUKOS WA GPL ALIYEKO MARASIBORA-TARIME

Leave A Reply