The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Mama Shigongo Waagwa Nyumbani, Nyakato Mwanza – Video

 

MWILI wa marehemu mama mzazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo, Bi. Asteria Kahabi Kapela iumewasili nyumbani kwake Nyakato, Mecco jijini Mwanza leo Jumatatu, Julai 30, 2018 ukitokea jijini Dar es Salaam ambako umauti ulimkuta.

Baada ya kufikishwa nyumbani hapo, mwili wa Bi. Asteria Kapela umefanyiwa maombi nyumbani kwake hapo kisha kuagwa na ndugu jamaa na marafiki na baadaye kupelekwa katika Kanisa Katoliki la Familia Takatifu, Nundu jijini humo kwa ajili ya maombi na kuagwa.

Mwili wa marehemu Asteria aliyeaga dunia Julai 27, katika Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI) Muhimbili jijiniu Dar es Salaam alikokuwa amelazwa, unatarajiwa kusafirishwa kesho Jumanne kwenda kijijini kwao, Bupandwamhela, Buchosa Sengerema ambako utazikwa Jumatano.

MWANZA: Kuagwa kwa Mwili wa Mama Shigongo

Comments are closed.