The House of Favourite Newspapers

Njombe: Mwili wa Marehemu Wafukuliwa – Video

0

IKIWA ni siku chache tu baada ya Jeshi la Polisi Mkoani Njombe kutangaza kupatikana kwa baadhi ya viungo vya mwili wa mfanyabiashara wa vitunguu mkazi wa Morogoro, ndugu wa mfanyabiashara huyo wamefika Njombe na kulazimika kufukua mwili wa ndugu yao na kuusafirisha kwenda kuuzika nyumbani kwao.
Mfanyibiashara huyo ambaye ametambulika kwa jina la Jackson Charles ambaye ni mkazi wa Kilosa Mkoani Morogoro, alipotea tangu Oktoba 22, 2021, Wilayani Wanging’ombe na baadaye baadhi ya viungo vya mwili wake vilipatikana katika msitu wa Ngaramaro, Kijiji cha Mtapa Wilayani humo.
Wakizungumzia tukio hilo, Viongozi wa Kata ya Kidugala Wilaya ya Wanging’ombe ambako Marehemu alikuwa akifanyia biashara wamesema mwili wa Charles ulikutwa msituni ukiwa umeharibika na baaadhi ya viungo vikiwa havipo.
Ndipo Serikali ikachukua jukumu la kuuzika papo hapo msituni mnamo Desemba 5, 2021 kutokana na mwili huo kuharibika vibaya. Tayari myu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kutokana na tukio hilo.

Leave A Reply