The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Misanya Bingi Waagwa Dar, Kuzikwa Dodoma -Video

MHADHIRI wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) ambaye pia aliwahi kuwa mtangazaji maarufu wa Radio One, Dkt. Misanya Dismas Bingi (47) aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki mwili wake umeagwa leo na kusafirishwa kwenda Dodoma atazikwa kesho katika eneo la Miyuji nje kidogo ya jiji la Dodoma.

Mwili wake umeaagwa katika Kanisa Katoliki Makongo Juu, ambapo baadhi ya wahadhiri walimwelezea kama mtu aliyeipenda kazi yake na mcheshi kwa kila mtu.

Akizungumza kwenye ibada ya kumwombea marehemu, Padre Steven Kaupe aliwataka waombolezaji kutoogopa kifo kwa vile kimewekwa kwa ajili ya binadamu.

“Tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kutuletea Misanya na kumshukuru pia kwa kumchukua,” alisema.
Marehemu Dk Misanya ameacha mke na mtoto mmoja na mwili wake uliagwa na mamia ya wananchi wakiwamo wafanyakazi wenzake wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Comments are closed.