The House of Favourite Newspapers

Mwinyi Afunguka Makamba Kuweka Picha Yake Mtandaoni – Video

Rais mstaafu wa awamu ya oili Ali Hassan Mwinyi na January Makamba.

RAIS mstaafu wa awamu ya pil,i Ali Hassan Mwinyi, amesema hajafurahishwa na kitendo cha aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba,  kutumia mitandaonipicha waliyopiga pamoja muda mfupi baada uteuzi wake kutenguliwa na Rais Magufuli.

 

Katika picha hiyo, ambayo January aliiweka muda mchache baada ya rais kutengua uteuzi wake ikimuonyesha yeye na Mwinyi wamekaa kwenye viti viwili tofauti,  aliandika:

“Kwa kweli nimeyapokea mabadiliko yaliyofanywa kwa moyo mweupe kabisa-kabisa. Nitasema zaidi siku zijazo.”

 

Mwinyi amesema hakuona ubaya wa picha ile na wala hakuchukizwa nayo kwa sababu watu wengi wanaokwenda kumuona humuomba picha ya ukumbusho lakini kilichomshangaza ni kitendo cha kutumia picha hiyo katika kipindi hiki.

 

“Kwa kweli sikupenda kuona picha ya namna ile katika mazingira haya, ile ni picha ya kawaida maana watu wengi wanakuja kuniona na tukishamaliza kuzungumza wanasema tupate ukumbusho na tumefanya sana kwa mtu mmoja-mmoja na kwa watu wengi sana kwa hiyo nimestaajabu nilipoona imewekwa wakati huu.

 

“Kijana yule ameandika kitabu na aliniomba nimsaidie kuandika dibaji, inawezekana alifanya kama kushukuru lakini silaumu wala sioni vibaya ila kwa nini ikawe katika mazingira haya wakati maji yamekorogeka?

 

”Ile picha ni ya zamani lakini mambo yametokea leo na huko zamani tulikuwa na sababu ya kufanya hivyo kwa sababu na mimi nilishika nafasi hii lakini pia kulikuwa na uhusiano wa kitabu chake alichokiandika maana si cha sasa hivi, kiliandikwa zamani lakini kwa nini ikawa sasa hivi?  Hili kidogo limenishtua,” amesema Mwinyi.

Comments are closed.