KAMA UNAHONGA ILI UPENDWE UMECHELEWA SANA , SOMA HII!

Ndugu zangu huko mtaani tunakoishi kuna watu ambao wamekuwa wakitumia nguvu kubwa sana kuhakikisha wanawapata wale ambao wametokea kuwapenda. Unamkuta mwanaume f’lani katokea kumzimikia msichana flani, anatumia maneno matamu, anatumia pesa na kila aina ya ushawishi kuhakikisha anampata. Hiyo imekuwa ikifanyika sana mtaani. Wapo wanaume ambao nawajua wametumia pesa zao kuhonga hadi zimeisha lakini

hawakufanikiwa kupata penzi la kweli. Wapo wafanyabiashara wengi tu ambao wametumia sehemu kubwa ya faida na wengine wakatumia mpaka mtaji kuwapa wanawake waliotokea kuwapenda lakini mwisho wa siku waliambulia patupu. Wengine wakahonga magari na vitu vingine vya thamani lakini kuonesha kuwa penzi la kweli haliwezi kupatikana kwa kutoa kitu, waliishia kunawa tu. Achilia mbali hao wanaume, wapo wanawake ambao nao wamekuwa wakitumia njia mbalimbali kuwashawishi wanaume wawapende.

Unamkuta mwanamke na pesa zake anadiriki kumpa mvulana kila kitu ili mradi awe naye na apate ile furaha anayoihitaji. Kimsingi wengi wamekuwa wakitumia njia za kulazimisha wapendwe bila kujua kwamba, kama hawapendwi hata watoe nini hawawezi kupendwa! Nalazimika kuyasema haya baada ya wiki iliyopita kuzungumza na mmoja wa wasomaji wangu aliyejitambulisha kwa jina moja la Nadhifa, mkazi wa Morogoro ambaye alinipa kisa cha kusikitisha sana.

Huyu ni msichana ambaye anatokea kwenye familia yenye uwezo kifedha lakini alichokuwa anakikosa ni penzi la kweli kutoka kwa mwanaume aliyempenda. Kwa maelezo yake anadai alitokea kumpenda kijana mmoja, aliamini huyo ndiye mume wa maisha yake. Alichokosea sasa ni kwamba, baada ya kujua kwamba analo penzi la dhati kwa mwanaume ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alianza kumpa zawadi za hapa na pale, wakati mwingine pesa. Mwanaume naye kama walivyo wanaume wengi wa mjini kupenda mteremko, alipobaini kuwa binti huyo

kamzimia, akawa anamkubalia kuwa na yeye anampenda kumbe ni usanii mtupu. Basi binti wa watu akajiaminisha kuwa amepata mwanaume, akajiachia. Alichokuwa akifanya Nadhifa ni kuhakikisha kila anachohitaji mwanaume huyo anampatia. Akakosea sana pale mwanaume huyo alipomtaka ampe mapenzi kinyume na maumbile na kumkubalia akijua ni njia ya kumshika.

Hapo ndipo alipoharibu na kwa kuwa mwanaume yule alikuwa hana mapenzi ya kweli, akaanza kumfanyia kila aina ya vituko. Si alijua hawezi kuachwa? Kwa hiyo mpaka sana uhusiano wao wao upo upo tu. Mpenzi msomaji wangu, hili ni kosa ambalo watu wengi wanalifanya. Tunatumia nguvu kubwa hata kufanya yasiyostahili eti ili kuwapata na kuwashika wale ambao tumetokea kuwapenda. Ukweli ni kwamba, anayekupenda wala huwezi kutumia nguvu kubwa kumpata wala kumshawishi asikuache.

Mwanamke huwezi kumzuia mpenzi wako asikuache kwa kumpa mapenzi kinyume na maumbile. Huko ni kujidhalilisha na kujishusha thamani. Ni hayo tu kwa leo, tukutane tena wiki ijayo kwa mada nyingine.


Loading...

Toa comment