The House of Favourite Newspapers

Mwizi Avunja Nyumba, Amuogesha Mtoto Kabla Ya Kuiba

MWANAMKE mmoja anayeishi Ohio nchini Marekani, amewaeleza polisi kuwa aliamka ghafla usiku wa manane na kukuta mvamizi akimuogesha mtoto wake wa kiume mwenye miaka miwili.

 

Areica Hill amesema kuwa aliamshwa na mbwa wake aliyekuwa akibweka ndipo alipotoka na kwenda chumbani kwa mwanaye na kumkuta mwanamke mwingine akimuogesha mtoto.

 

Anasema alianza kupigana naye kabla ya kuwapigia polisi simu kwa ajili ya msaada zaidi na walifika na kumkamata Elizabeth Hixon (22).

 

Binti huyo ameshtakiwa kwa uvamizi na mahakama imemuachia kwa dhamana na kesi hiyo itasikilizwa tena siku ya Ijumaa tarehe 25 Oktoba, 2019.

Comments are closed.