The House of Favourite Newspapers

Mzee Akilimali: Uchaguzi Utamaliza Shida za Yanga

KATIBU wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali, amewataka mashabiki na wanachama wa Yanga kutokukubali kuchanga pesa zao kwa kuwa anaamini hazitokuwa katika sehemu salama.

 

Akilimali ametoa kauli hiyo ikiwa ni baada ya hivi karibuni klabu hiyo kutangaza mpango huo wa kuchangiwa na wanachama na mashabiki wa timu hiyo ya Jangwani.

Ikumbukwe pia, msimu uliopita Yanga SC ilianzisha mfumo huo wa kuomba michango kwa wanachama lakini hawakuwaeleza kuwa walipata shilingi ngapi.

 

Akizungumza na Championi, Mzee Akilimali alisisitiza kuwa si vyema kwa Yanga kuendeshwa kwa mfumo huo na badala yake viongozi waliopo madarakani kujiuzulu ili kufanya mabadiliko ya kiuongozi ambayo anaamini ndiyo suluhisho ya hayo yote.

“Nawaomba wana Yanga hasa wenye uchungu na kuipenda timu yao wasitoe hata senti moja kwa sababu hakuna usalama wa kile kitakachotolewa, nasema haya kwa akili sana na kwa uchungu sana.

 

“Ni bora viongozi walioko madarakani sasa wajiuzulu wote na kuipisha Yanga iingie katika uchaguzi wa viongozi wapya ambao mfumo huo wa kisasa umekuwa ukitumika na Yanga tangu mwaka 2008, hilo ndilo litakuwa suluhisho,” alisema Mzee Akilimali.

Warren Gerson, Dar es Salaam

Comments are closed.