The House of Favourite Newspapers

Mzee wa Upako Amvaa Lowassa

mzee-wa-upako3upakoStori: Na Mwandishi, Wikienda

DAR ES SALAAM: Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ ame­tumia ibada aliyoifanya kanisani kwake, Ubungo-Kibangu jijini Dar jana, kumvaa aliyekuwa Waziri Mkuu na Mgombea Urais Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa kuwa hawezi kuwa rais mwaka 2020.

Mzee wa Upako alisema kuwa, anajua anashambuliwa na baadhi ya wachungaji na watu wengine wakiwepo Chadema kwa sababu ya Rais John Pombe Magufuli kumjengea Barabara ya Kibangu jijini Dar hivyo kuona kama anakubalika kwa rais.

“Mimi nashangaa chuki za nini au sababu ni Rais John Pombe Magufuli kuijenga Barabara ya Kibangu? Rais hakujenga bara­bara hii na kusema ni yangu bali amewajengea wakazi wa Kibangu, ingekuwa ni yangu, ningekuwa naweza kukatisha ushuru kwa wapiti njia.

Lowassa

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa

“Najua wanaonichafua, Chadema wanahusika kabisa kwenye hili, hivi unadhani Lowassa anaweza kuwa raisi mwaka 2020 kwa akili yako? Kuwa na wabunge wengi bungeni wanaweza, lakini rais ni ndoto ya mchana. Hata kama nitakuwa nimeaga dunia, Lowassa hawezi kuchukua nchi hii.

“Namshangaa sana Low­assa kutaka ving’ora, mbona vingora alishapigiwa sana wakati akiwa waziri mkuu, nakumbuka kuna siku ni­likuwa eneo la Kamata (Dar), mara askari wa usalama barabarani akasimami­sha magari likiwemo na la kwangu, nikauliza kulikoni nikaambiwa Waziri Mkuu, Lowassa anapita. Sasa nini kingine anakitaka?

“Siku Lowassa akifariki dunia ni lazima atapigiwa mizinga kumi na nane kwa heshima kubwa aliyonayo katika nchi hii, sasa ana­taka heshima gani nyingine jamani?

“Mimi sikumtabiria Rais Magufuli, alitabiriwa na TB Joshua, sasa uhasama una­toka wapi jamani? Mimi sina kosa wananionea bure tu.

“Nampongeza sana Rais Magufuli, sina shaka na uongozi wake kabisa, kamatia hapohapo (akaanza kuimba Wimbo wa Kundi la Navy Kenzo wa Kamatia Chini) ‘kamatia chini, kama­tia chini…’. Si kweli kwamba Rais JPM ni mkali, hapana, ni mtu mwema, mpole, mpenda amani na haki na anataka kila mwananchi awe na ma­fanikio kupitia nchi yake.

Comments are closed.