The House of Favourite Newspapers

Simba Uso Kwa Uso na Yanga Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi, Yaizamisha Jang’ombe Boys bao 2-0

simba-1

Kikosi cha Jang’ombe Boys kilichoanza leo dhidi ya Simba katika Uwanja wa Amaan.

simba-25

Kikosi cha Simba kilichoanza dhidi ya Jang’ombe Boys.

simba-26

Mshambuliaji wa Simba Juma Liuzio akifanya yake.

simba-2 simba-3 simba-5 simba-6

Mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo (mwenye namba 11) akifanya yake dhidi ya wachezaji wa Jang’ombe Boys.

simba-7

Mshambuliaji wa Simba, Pastory Athanas akimiliki mpira mbele ya  mchezaji wa Jang’ombe.

simba-8 simba-9 simba-10

Mchezo ukiendelea.

simba-13

Mavugo akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza huku akifuatwa na Shiza Kichuya.

simba-14 simba-15

Wachezaji wa simba wakiendelea kushangilia.

simba-17

Kichuya akipambana.

simba-18 simba-19

Wachezaji wa Simba na Jang’ombe wakiwania mpira.

PICHA: Musa Mateja/GPL

LEO Simba imemaliza mchezo wao wa mwisho wa Kundi A katika michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kuichapa Jang’ombe Boys mabao 2-0 na kufikisha pointi kumi wakiwa kileleni mwa kundi hilo.

Mabao ya Simba leo yamefungwa na mshambuliaji wao wa kimataifa, Laudit Mavugo raia wa Burundi katika dakika za 11 na 53.

Kwa matokeo hayo, Simba imetinga nusu fainali ya michuano hiyo na sasa itapambana na Yanga, keshokutwa Jumanne.

Ikumbukwe kuwa, Yanga ilitinga nusu fainali kutokea Kundi B baada ya kumaliza ikiwa ya pili na pointi sita nyuma ya vinara wa kundi hilo, Azam waliomaliza na pointi saba.

HUSNA SAJENT: NIMEZAA NA CHAZ BABA NA GABO

Comments are closed.