The House of Favourite Newspapers

Mzungu Simba Awapa Makavu Nyota Wake

0

SVEN Vanderbroeck amesema kuwa wachezaji wake walicheza chini ya kiwango kipindi cha pili jambo lililofanya kuruhusu kufungwa mabao mawili kipindi cha pili licha ya wao kuanza kuifunga Yanga kwenye mechi iliyochezwa juzi Uwanja wa Taifa.

 

Sven alikuwa akiiongoza Simba kwa mara ya kwanza kwenye dabi ya Kariakoo na kushuhudia mabao mawili waliyoanza kuyafunga Simba yakipinduliwa na wapinzani wao Yanga ndani ya dakika saba za kipindi cha pili.

 

“Sijafurahishwa hata kidogo na tukio ambalo nimelishuhudia, kufungwa mabao mawili ndani ya dakika saba hili jambo ni baya na linaumiza, wachezaji hawajafanya kile ambacho nilitarajia mwanzo.

 

“Ninaamini kwamba walishindwa kujituma na kulinda ushindi waliopata kutokana na kujiamini kupita kiasi na kusahau kwamba mpira unaendelea, nitakaa na wachezaji wangu kuzungumza nao kwani hawajafanya vizuri kuruhusu mabao waliyoanza kufunga,” alisema Sven.

 

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salam

Leave A Reply