The House of Favourite Newspapers

NACTE Yafuta Leseni ya Vyuo vya Ufundi 26

baraza-la-taifa-la-elimu-ya-ufundinacte

 

  • Nacte  yafuta leseni ya vyuo vya ufundi 26
  • 20 vyasimamishiwa programu zisizosajiliwa na baraza hilo
  • 2 vyasimamishwa kwa kutokuwa na usajili

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limevifungia vyuo vya ufundi 26 kutokana na makosa mbalimbali, ikiwamo kushindwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na kutoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Kaimu Katibu mtendaji wa NACTE,    Dkt. Adolf Rutayuga, alisema kuwa wamekuwa wakifuatilia vyuo vya ufundi ili kutathmini kama vinafuata viwango vya ubora wa kitaaluma vilivyowekwa na NACTE katika kutoa mafunzo. 

“Kama ilivyoelezwa katika sheria za Usajili na Kanuni za leseni, kutozingatia  matakwa yoyoye yaliyowekwa na NACTE ni kosa kisheria. Kanuni zinasema kuwa hatua kali zinawezakuchukuliwa kwa kila kosa. Kulingana na matokeo  ya ufuatiliaji uliofanywa na timu maalumu, Baraza lina uwezo wa kuchukua hatua dhidi ya taasisi au vyuo vinavyoshindwa kutekeleza kanuni zilizowekwa,” alisema.

Alisema kuwa baada ya kufanya utafiti wao, wamebaini vyuo 26 vilishindwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na NACTE katika cheti cha usajili, huku vyuo 20 vikitoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa chini ya idara isiyotambulika,wakati vyuo viwili vikiwa na vituo vya satellite/Kampasi ambavyo navyo havijathibitishwa na chombo husika.

“Baraza linaufahamisha umma kwamba limechukua hatua mbalimbali kwa vyuo vya ufundi 48 kutokana na makosa mbalimbali, yaliyofanywa na vyuo hivyo ambapo limesitisha vyeti vilivyotolewa kwa vyuo 20 ambavyo vimeshindwa kuzingatia masharti yaliyowekwa kwenye Cheti cha Usajili.

“Uamuzi huu umefanywa kwa mujibu wa Kanuni ya 20 ya Usajili wa Vyuo vya Ufundi ya mwaka 2001,” alisema.

Rutayuga alisema kwamba vyuo vilivyofutiwa usajili kutokana na kosa la kutoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa chini ya idara isiyotambulika ni 26.“Vyuo vya ufundi vinatakiwa kupata kwa idhini ya Baraza kabla ya kuanza kutoa mafunzo yoyote. Idhini hiyo inahusu uthibitisho wa mtaala kwa ajili mafunzo yaliyokusudiwa na utambuzi wa idara iliyopangwa kutoa mafunzo hayo,” alisema. 

Juu ya vyuo vyenye vituo vya setelite, kampasi, Dkt.Adolf Rutayuga alisema kuwa Baraza linahitaji mafunzo kutolewa katika vituo vilivyosajiliwa/kampasi za vyuo vikuu baada ya kuthibitishwa kwamba vinastahili kutoa mafunzo. 

“Hata hivyo, taasisi mbili zimebainika kutoa mafunzo katika vituo vya satellite/vyuo vikuu ambavyo havijasajiliwa na Baraza na hivyo kuadhibiwa. Vyuo hivyo navyo vimefutiwa leseni,” alisema Rutayuga.

NACTE ni bodi iliyoanzishwa kisheria chini ya Sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, kifungu cha 129, kusimamia na kuratibu utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo nchini Tanzania.  Chini ya sheria hiyo, ili kufikia na kudumisha hali ya mtoa mafunzo, vyuo vyote vinatakiwa viwe vimesajiliwa, vibali na kuwa mitaala iliyopitishwa na baraza. Vyuo haviruhusiwi kuanza kutoa kuanza kutoa huduma yoyote ya mafunzo bila idhini ya baraza.

Jedwali 1: Vyuo vya Ufundi vilivyofutiwa usajili

S/N

CHUO

1

Institute of Management and Development Studies – Iringa

2

Green Hill Institute – Mbeya

3

Institute of Business and Social Studies – Mbeya

4

Loyal College of Africa – Mbeya

5

Mbeya Training College – Mbeya

6

Mbengwenya College of Business and Information Technology –Mbinga

7

New Focus College – Mbeya

8

Shukrani International College of Business and Administration –  Mbeya

9

Majority Teachers College – Mbeya

10

Rukwa College of Health Sciences – Sumbawanga

11

MAM Institute of Education – Mbeya

12

Belvedere Business and Technology College – Mwanza

13

Geita Medical Laboratory Sciences and Nursing Training College – Geita

14

Global Community College – Geita

15

Muleba Academy Institute – Muleba

16

St. Bernard Health Training Institute – Katoro, Geita

17

Victoria Institute of Tourism and Hotel Management – Mwanza

18

Gisan Institute of Health Sciences – Mwanza

19

Dar es Salaam Institute of Business Management – Dar es Salaam

20

SAMFELIS College of Business Studies – Dar es Salaam

21

Ellys Institute of Technology – Bunda, Mara

22

Tanzania Institute of Chartered Secretaries and Administrators – Arusha

23

Emmanuel Community College – Kibaha

24

Modern Commercial Institute – Dar es Salaam

25

Marian College of Law – Dar es Salaam

Jedwali 2: Vyuo vya Ufundi vinavyotoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa

S/N

CHUO

MAFUNZO

1

MISO Teachers College – Mafinga

Competence Building Network (CBN) – a Certificate in Early Childhood Education

2

Tusaale Teachers College – Mafinga

Competence Building Network (CBN) – a Certificate in Early Childhood Education

3

The St. Joseph’s College Institute of Business and Management (SJCIBM) – Morogoro

 

4

The Golden Training Institute – Dar es Salaam

 
 
 
 
 
 

5

Nkrumah Mkoka Teachers College – Kongwa, Dodoma

 

6

National Institute of Agriculture (Chuo cha Kilimo cha Taifa) – Arusha

 

7

Musoma Utalii Training College – Musoma

 

8

Mwanza Polytechnic Institute – Mwanza

 

9

Mwanza Polytechnic Institute – Maswa

 

10

Ruter Institute of Financial Management – Mwanza

 

11

Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Mwanza

 

12

Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Geita

 

13

Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Bukoba

 

14

Singni International Training Institute – Bukoba

 

15

Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Kahama

 

16

Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Simiyu

 

17

Richrise Teachers College – Geita

 

18

Twiga Training Institute – Musoma

 

19

Zoom Polytechnic Institute – Bukoba

 

20

St. Thomas Training College – Shinyanga

 

Jedwali 3: Vyuo vya Ufundi vyenye Vituo vya Satellite / Kampasi

S/N

CHUO

1

MISO Teachers College – Mafinga

2

Rungemba Teachers College – Mafinga

halotel-2

Comments are closed.