NAFASI YA KAZI: MAOFISA MAUZO, GLOBAL PUBLISHERS, DAR

GLOBAL PUBLISHERS AND GENERAL ENTERPRISES LIMITED, ni kampuni ya uchapishaji magazeti na wamiliki wa Global TV, Global Radio na mitandao yake ya kijamii inayofuatiliwa na watu wengi. Kampuni inawatafuta MAOFISA MAUZO wenye uzoefu wa kutafuta masoko kwenye vyombo vya habari (Utafutaji wa Matangazo), mwenye ujuzi na sifa zifuatazo:

SIFA:

VIJANA wanaotafutwa, wawe wameshawahi kufanyakazi kwenye vyombo vya habari idara ya matangazo au wawe wameshawahi kufanyakazi katika Kampuni za Mawakala wa Utangazaji (Advertising Agency), kwa muda usiopungua miaka miwili. Vijana wanaotafutwa wawe na uwezo mkubwa wa kuongea na kuandika kwa ufasaha lugha ya Kiswahili na Kiingereza na wawe wanaishi Dar es Salaam. Tunakaribisha pia maombi ya watu wenye uzoefu na masuala ya matangazo kuomba kama FREELANCERS, ndani na nje ya Dar es salaam.

Mwisho:

Kama unafikiri unakidhi vipengele vyote vilivyoainishwa hapo juu, tuletee ofisini barua yako ya maombi ya kazi haraka, iliyoambatana na CV yako pamoja na vivuli vya vyeti vyako, kwa:

MENEJA MKUU,

S.L.P 7534,

DAR ES SALAAM

Au  wasilisha mwenyewe ofisini kwetu, Sinza Mori (Global Group House). Simu: 0715 288627. email: uwazihabari@gmail.com. Mwisho wa kupokea maombi ni 31 Julai,  2019.

 

 

 


Loading...

Toa comment