The House of Favourite Newspapers

UCHAGUZI SINGIDA: MGOMBEA CCM APITA BILA KUPINGWA

Miraji Mtaturu

MGOMBEA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Miraji Mtaturu,  amepita bila ya kupingwa katika hatua za awali za matayarisho ya uchaguzi mdogo ambao ungefanyika kwenye Jimbo la Singida Mashariki, baada ya wagombea 12 wa vyama vya upinzani kutorejesha fomu.

Uchaguzi huo mdogo ulikuwa ufanyike Julai 31, mwaka huu,  kufuatia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Tundu Lissu kuvuliwa ubunge.

Comments are closed.