The House of Favourite Newspapers

NAI AMTOLEA POVU LYNN

Nai Kisa ‘Nai’

MUUZA sura kwenye video Bongo, Nai Kisa ‘Nai’ ameibuka na kumtolea povu muuza sura mwenzake, Irene Hillary ‘Lynn’ kwamba hana tabia ya kudanga kwa wanaume ili apate pesa kama mwenzake huyo.  

 

Akipiga stori na Risasi Vibes, Nai alimtaka Lynn kuacha kumzungumzia vibaya katika biashara zake ndogondogo anazozifanya kwa ajili ya kujipatia kipato na badala yake afanye mambo yake yanayomuhusu.

 

“Nashangaa kwa nini huyo Lynn anadharau biashara yangu, kitu ambacho sikipendi anaona kazi zangu hazina maana kwa kuwa amezoea kudanga kwa wanaume ndiyo apate pesa, kwa hiyo naomba aache kudharau biashara yangu kwa sababu ndiyo inanifanya mimi niwe hapa,” alisema Nai ambaye anafanya biashara ya kupamba watu ‘make up’. 

Risasi Vibes ilimtafuta Lynn ili kutaka kujua anazungumziaje kauli ya Nai ambapo aliongea kwa kifupi na kusema hana muda wa kuzungumzia ishu kama hizo.

Comments are closed.