The House of Favourite Newspapers

Nai Awakataa Gigy, Amber Lulu

0


VIDEO Vixen matata na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nairath Ramadhani ‘Official Nai’ amefunguka kuwa mtu aliyemleta mjini ni msanii mwenzake Sharif Thabeet ‘Darassa’ na si mwingine yeyote.

Majibu hayo yamekuja baada ya hivi karibuni kuzushiwa kwamba aliyemtambulisha Nai kwenye tasnia ni Gift Stanford ‘Gigy Money’ pamoja na Amber ambapo mrembio huyo amedai kuwa Darassa ndiye aliyeweza kumtambulisha kupitia Wimbo wa Maisha na Muziki.

“Nashangaa watu wanavyoniambia kwamba eti Gigy na Amber Lulu ndiyo wamenileta mjini who is Gigy (Gigy ndiyo nani) kwenye maisha yangu labda niwaambie tu kitu ambacho hamkijui mtu aliyeweza kunitambulisha kwenye hii tasnia ni Darassa na alinitambulisha kupitia muziki wake wa Maisha na Muziki aliofanya na Ben Pol,” alisema Nai

Leave A Reply