The House of Favourite Newspapers

NAI, FAHYMA NDANI YA BIFU ZITO

Fahyma

MZAZI mwenzake na msanii wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ Fahyma ameingia katika bifu zito na Video Vixen Bongo, Nai kisa kikiwa ni kugombea jina la Tanzania Baby.  

Ishu nzima ilianzia mitandaoni baada ya Nai kuibuka na kudai kukopiwa jina hilo ambalo yeye alikuwa akilitumia tangu mwaka 2016.

Akizungumza na Ijumaa, Nai alisema anashangaa kumuona Fahyma akijiita hilo jina la Tanzanian Baby wakati watu wote wanajua ni yeye hivyo aache kujisumbua kwa kutaka jina ambalo si lake.

 

“Mimi nilianza kujiita Tanzanian Baby tangu mwaka 2016 nilipoanza tu kufanya u-video Vixen na kila mtu analijua hilo, sasa yeye kaanza kujiita juzi tu baada ya kuona Diamond kaliimba hilo jina kwenye wimbo wake wa ‘Eneka’ halafu namshangaa jinsi anavyopaniki vitu visivyokuwa na maana, atulize shobo mimi ndiyo Tanzanian Baby,” alisema Nai.

Ijumaa pia lilimcheki Fahyma kujua kwa upande wake ambapo simu yake iliita bila kupokelewa na hata alivyotumiwa ujumbe mfupi ulionesha kupokelewa bila majibu. Bado ataendelea kutafutwa japokuwa alishakaririwa akisema yeye ndiyo Tanzanian Baby.

Comments are closed.