The House of Favourite Newspapers

Nai: Mwanaume Akitaka Nimposti, Aninunulie Ferari

0

 MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva anayekuja kwa kasi, Hunai Ramadhani ‘Official Nai’ amesema kuwa mwanaume atakayetaka amposti labda amnunulie gari aina ya Ferari.

 

Akizungumza na RISASI VIBES, Nai ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Siyo Saizi Yao, amesema kuwa mpenzi atakayekuja kumuonyesha mitandaoni anatakiwa awe amefanya vitu vikubwa sana.

“Mpenzi nitakayekuja kumuonyesha inabidi awe amefanya vitu vikubwa sana kama ni nyumba awe amejenga ghorofa na kama ni gari basi awe amenunua Ferari ndiyo nitaweza kumposti lakini sioni faida ya kumuonyesha mtu ambaye ajanifanyia kitu kikubwa chochote,” alisema Nai

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply