The House of Favourite Newspapers

Waziri Kanyasu: Kuleni Nyama ya Mamba ni Tamu

0

NAIBU Waziri wa  Maliasili na Utalii, Constantine John Kanyasu,  amesema kuwa mamba ana nyama tamu na ngozi yake ni biashara nzuri huku akiwataka wanaohitaji kuvuna mamba kuomba vibali kwa maafisa wanyamapori.

 

“Mamba ana nyama tamu sana, anzeni kula nyama yake badala ya kutegemea kitoweo cha samaki pekee” amesema.

 

Amefafanua kuwa licha ya nyama hiyo kuwa tamu,  kwanza mvunaji wa mamba aombe kibali kutoka kwa maofisa wanyamapori cha kuwavuna kinachotolewa kila Julai Mosi.

 

“Mbali na nyama yake kuwa tamu, lakini pia ngozi yake ni biashara yenye tija ndani na nje ya nchi,” amesema na kuongeza kuwa Serikali ina mpango wa kufungua mabucha yatakayouza nyama za wanyamapori katika maeneo mbalimbali nchini.

 

“Wizara imeanzisha utaratibu wa uwindaji wa ndani (resident hunting) ambapo nyama zitakazokuwa zikipatikana zitakuwa zikiuzwa kwenye mabucha hayo,” amesema.

 

Amesema hiyo itasaidia wananchi kupata nyama za pori kwa urahisi pale wanapokuwa na uhitaji. “Hivyo wawindaji watatakiwa kufuata taratibu za kuomba vibali kwa ajili ya kuwinda, ambavyo vitaainisha aina ya wanyama ambao watakwenda kuwawinda.”

Leave A Reply