The House of Favourite Newspapers

NALA Yapewa Leseni Ya Mtoa Huduma Za Malipo Na BOT, Yaahidi Kufanya Uwekezaji Wa Zaidi Ya Sh. Bilioni 2

0
Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Kampuni ya NALA, Benjamin Fernandes akionesha cheti walichopewa na BOT.

Dar es Salaam, Mar 27, 2023NALA imepokea leseni ya mtoa huduma kwa malipo kutoka Benki Kuu ya Tanzania, ikiwa ni matunda ya azma ya serikali ya Tanzania kuhamasisha uvumbuzi na teknolojia ili kufungua uchumi.

Muhtasari

NALA ni kampuni mashuhuri ya teknolojia ya malipo ya nchini Tanzania, ilifikia hatua kubwa katika dhamira yake ya kujenga mtandao thabiti wa malipo barani Afrika.

Kampuni hiyo imeidhinishwa na benki kuu ya Tanzania kama mtoa huduma ya malipo, ambayo itawezesha muunganiko wa moja kwa moja na benki pamoja na waendeshaji wa huduma za fedha kwa njia ya mitandao ya simu za mkononi, kama vile Mpesa.

Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Kampuni ya NALA, Benjamin Fernandes. Kushoto ni Maofisa wa Kampuni hiyo Pepesa Sanga na kulia ni Thomas Vicen.

Leseni hii pia itawezesha kampuni kuanza kutengeneza bidhaa za ziada za kidijitali ambazo zitaongeza ujumuishaji wa malipo, kufanya huduma za malipo ziwe nafuu zaidi na za kuaminika kwa biashara na matumizi ya kawaida.

Utangulizi

NALA, kampuni ya malipo ya kimataifa iliyozaliwa nchini Tanzania, ilitanua wigo wake kutoka Uingereza na Marekani hadi Ulaya mapema mwaka huu. NALA imekua kwa kasi kuanzia kijiografia, utofautishaji wa bidhaa na uboreshaji wa miundombinu iliyopo.

Mara baada ya NALA kuzinduliwa katika Umoja wa Ulaya, kampuni hiyo ilipokea leseni yake ya mtoa huduma za malipo nchini Tanzania. Hii ni hatua kubwa kwa kampuni hiyo kwani inatoa nafasi ya kuboresha huduma na kuongeza mpya, kama vile; malipo ya kibiashara, huduma za wafanyabiashara na malipo ya nje kutoka Tanzania, pamoja na ushirikiano wa moja kwa moja na benki za ndani na kampuni za mawasiliano.

Leseni hii imetolewa, ikiwa ni muendelezo wa juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwainua vijana, lakini pia kuweka mazingira rahisi ya kiuwekezaji kwa ujumla, ili makampuni mengi kama NALA yaweze kuwekeza nchini.

NALA inaendeleza shughuli zake za kiutendaji nchini, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono maono ya Rais wetu, ya kujenga Tanzania iliyoinuka kiugunduzi pamoja na teknolojia kwa ujumla wake.

Akizungumza na waandishi wa habari, mwanzilishi na mkurugenzi wa kampuni ya NALA, Bw. Benjamin Fernandes amesema:

“Malengo mawili makubwa ya NALA kutokea mwaka jana yamekuwa kuwezesha ushirikiano wa moja kwa moja kwa benki na kampuni za mawasiliano ya simu, kukabiliana na changamoto ambazo wafanyabiashara wanakabiliana nazo katika kuhamisha fedha kuvuka mipaka ya nchi.

Tumefanya kazi kwa karibu pamoja na Benki Kuu ya Tanzania ili kukamilisha hatua zinazofaa za kupokea leseni yetu kama mtoa huduma wa malipo. Kwa leseni hii mpya mkononi, NALA inapata nafasi na uwezo wa kuendelea na malengo yetu, kubwa likiwa kufanya uwekezaji wenye thamani ya zaidi ya Bilion 2 za kitanzania ili kujenga miradi yetu mikubwa zaidi kuwahi kutokea katika soko letu la hapa nyumbani Tanzania.”

Baadhi ya wachapakazi wa NALA katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mkutano na wanahabari jijini Dar leo.

NALA inapatikana nchi nyingi za Ukanda wa Afrika na Ulaya, unaweza kuipakua kwenye simu yako kupitia App Store au Play Store.

Licha ya chaguzi nyingi za kutuma pesa Afrika kutoka ng’ambo, bara hili bado limeendelea kuwa mahali pa gharama kubwa zaidi kutuma pesa. Benki ya Dunia inakadiria wastani wa ada za kutuma fedha Afrika kuwa 9%.

Zaidi ya hayo, chaguo nyingi zilizopo ni pamoja na ada zilizofichwa ambazo hufanya iwe vigumu kutambua gharama halisi ya kutuma pesa. NALA inajitahidi kubadilisha dhana ya zana za kifedha kwa Waafrika kwa kutoa huduma za haki na uwazi ili kuwawezesha watu kudhibiti fedha zao.

Kuhusu NALA:

NALA ni kampuni ya malipo ya Kiafrika na programu ya kutuma pesa ambayo hukuwezesha kufanya malipo salama na ya kuaminika kutoka Ulaya, Uingereza na Marekani hadi Afrika kwa sekunde chache.

Kampuni hiyo ina dhamira ya kuongeza fursa za kiuchumi katika bara la Afrika na miongoni mwa wanadiaspora duniani kote. Kuunda masuluhisho ya kifedha yanayoendeshwa na jumuiya, hurahisisha kufanya malipo ya kila siku na kuongeza fursa za biashara katika Afrika inayokua duniani.

Malipo barani Afrika yamejengwa kwa 1%. NALA inatamani kuleta teknolojia ya malipo ya karne ya 21 barani Afrika ili kuunda njia za malipo za gharama ya chini na zinazotegemeka sana ambazo marafiki, familia na wafanyabiashara wanaweza kutumia. Ikiwa malipo ni rahisi, ya kuaminika, na yanapatikana kwa kugusa kitufe, chochote kinawezekana.

Kwa kujenga njia za malipo na miundombinu, NALA itawezesha malipo ya haraka kwa bara la Afrika. Teknolojia yao imeundwa na wahandisi wa kiwango cha kimataifa kutoka duniani kote na tunajivunia kuhudumia jumuiya zote, kuanzia miji yenye shughuli nyingi hadi vijiji vyenye amani. Tumebahatika kushirikiana na jumuiya hizi katika safari hii pamoja.

Leave A Reply