The House of Favourite Newspapers

Kuondoa Vikwazo Viletavyo Athari Kwenye Ukoo – Video

0

KATIKA kipindi cha Darasa jana tarehe 29, June 2020, kupitia +255 Global Radio, walimu wa darasa maalumu lenye masomo yanayogusa maisha watu, wajasiriamali Eric Shigongo  na Rodrick Nabe wametoa somo kuhusu ‘namna ya kuondoa vikwazo vinavyoweza kuleta athari kwenye ukoo’

 

Akizungumzia namna ya kuondoa vikwazo vinavyoweza kuleta athari kwenye ukoo, Shigongo ameainisha mambo kadhaa ambayo ni lazima mtu ayazingatie katika mchakato mzima.

 

Jambo la kwanza alilogusia ni ‘nia’ ya kuondoa vikwazo vilivyopo; ambayo ili mtu afanikiwe katika jambo hilo ni lazima awe na nia thabiti ya kuondoa vikwazo hivyo, na jambo la msingi  ni kuwa na nia ya kuvunja rekodi ya mafanikio waliyoyapata wazazi wake, kielimu, kiuchumi, n.k.

 

Alifafanua kuwa mtu akijiwekea nia ya kuvunja rekodi ya wazazi, itakuwa ni rahisi sana kuyafikia mafanikio makubwa kimaendeleo.

 

“Kuna baadhi ya matendo ambayo wazazi wakiyafanya, yanakuwa na athari za moja kwa moja kwenye kizazi chao, alisema Shigongo.

 

Naye Rodrick Nabe ameainisha mambo kumi ambayo yamekuwa yakijirudia kizazi hadi kizazi katika familia/koo nyingi; ambayo ni uvivu, uchoyo, kutokujielemisha, mahusiano mabaya, hofu iliyopitiliza, dhambi zinazotembea kizazi hadi kizazi, ulevi, madeni na umasikini.

Kwa maelezo zaidi ya ‘Darasa’  tazama Video hii hapa chini

Leave A Reply