The House of Favourite Newspapers

Nana Akufo-Addo Aapishwa Kuwa Rais wa Ghana

akufo 

GHANA: Viongozi kadha wa Afrika leo wamekusanyika katika Mji Mkuu wa Ghana, Accra, kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo, Nana Akufo Addo.

Maelfu ya wageni walialikwa kwenye sherehe katika Medani ya Uhuru mjini Accra.

nana-akufo-addo1Bwana Akufo Addo, aliyewahi kuwa wakili wa haki za kibinaadamu, alimshinda aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, John Dramani Mahama, katika uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita.

Madaraka yamekabidhiwa kwa kiongozi Akufo-Addo kwa njia ya amani, jambo linaloonekana kuwa mfano mwema wa demokrasi barani Afrika ambako katika baadhi ya nchi, viongozi hawataki kun’gatuka.

nana-akufo-addo

Baada ya kuapishwa kwa rais, sasa viongozi waliohudhuria sherehe hiyo, watajadili namna ya kuhakikisha kuwa Rais wa Gambia, Yahya Jammeh, anaondoka madarakani ambapo kiongozi huyo amekataa kustaafu ingawa alishindwa katika uchaguzi wa mwezi Desemba.

Comments are closed.