The House of Favourite Newspapers

Nandy ‘Amvuruga’ Naibu Spika

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson ameonyesha kuusifia wimbo wa ‘Kivuruge’ ulioimbwa na msanii wa Bongo Flava, Nandy huku akieleza kuwa kwa jitihada alizonazo msanii huyo atafika mbali.

Dkt. Tulia amesema kuwa kwa jitihada alizonazo msanii huyo atafika mbali na maudhui yaliyo katika wimbo huo ambao unamuelezea mwanamke anayelalamikia kusumbuliwa katika mapenzi.

“Kwa jitihada hizi natumaini utafika mbali zaidi, uvumilivu na nidhamu ni vya kuzingatia kwenda kwenye mafanikio. Wimbo wako Kivuruge tumeupokea kwa mikono miwili,” ameandika Dkt Tulia kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Wimbo huo kwenye mtandano wa YouTube unmetazamwa na watu 653,517 , ikiwa leo ni siku ya 9 tangu ilipowekwa kwenye mtandao huo.

Comments are closed.