The House of Favourite Newspapers

Nandy Atambulisha lebo Yake Mpya ya Muziki iitwayo The African Princess Label

0
Faustina Mfinanga almaarufu Nandy.

Staa wa kike wa Bongo Fleva, Faustina Mfinanga almaarufu Nandy ametambulisha lebo yake mpya ya muziki iitwayo The African Princess Label.

Utambulisho huo, utafuatiwa na tukio la kutambulishwa kwa msanii wa kwanza wa lebo hiyo, ambapo kupitia akaunti yake ya Instagram, Nandy ametupia picha akiwa ameshikana mkono na mwanadada ambaye hajaoneshwa uso, anayetajwa kuwa ndiye atakayetambulishwa rasmi Januari 19, 2023.

Nandy anakuwa msanii wa pili wa kike kuanzisha lebo yake, wa kwanza akiwa ni Vanessa Mdee ambaye alikuwa na lebo yake ya Mdee Music.

Nandy amesema kuwa lengo la kuanzisha lebo hiyo kuwasaidia na kuwainua wasanii chipukizi wa kike nchini na barani Afrika.

 

Ninayo furaha kubwa kuileta kwenu Rasmi THE AFRICAN PRINCESS LABEL…! 2023 lebel ambayo itahusisha wanawake tu! Kama tunavo ona industry ya watoto wa kike ni chache sana na uthubutu umekuwa ni mdogo so tunaimani na kuomba the African princess label itaongeza wingi wa vipaji vya watoto wa kike waliopo mtaaani wenye ndoto kubwa ya kuwa wanamziki!!

Leave A Reply