The House of Favourite Newspapers

Nay Afungukia Maajabu ya Wapo

0

Na Boniphace Ngumije| IJUMAA WIKIENDA| DAR ES SALAAM

MWANAMUZIKI Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ anayesumbua na Wimbo uitwao Wapo, hivi karibuni amefunguka namna wimbo huo ulivyomletea mafanikio ndani ya muda mfupi tangu auachie jambo ambalo kwake ni kama maajabu.

Akichonga na Over Ze Wikend, Nay alizidi kufunguka kuwa miongoni mwa mafanikio ambayo wimbo huo uliyompa misukosuko umempatia ni kubadilishwa lugha na ‘media’ mbalimbali za nje zikiwemo BBC na CNN ili dunia nzima iweze kuupata ujumbe alioulenga lakini pia shoo ambazo hazikatiki.

“Tofauti na nyimbo zangu zote, Wapo umenipa mafanikio sana. Naona ni kama maajabu maana kila wiki napiga shoo kuanzia tatu lakini pia umenifanya kuwa karibu na viongozi wa kiserikali na ambao hawapo serikalini. Lakini pia ni kujulikana zaidi nje ya nchi maana media za nje zimenizungumzia sana,” alimaliza

 

Yusuph Mlela Kimenuka ! Amtumbua Live Nay wa Wamitego, Aanika Siri Nzito

Leave A Reply