Nay: Kuhusu Nini, Ukweli Naujua Moyoni

MKALI wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amefunguka kuwa, baada ya kufanya kazi na mrembo anayekuja kwa kasi kwenye muziki, Nini, maneno yamekuwa hayaishi hivyo wamuache kwani ukweli anao yeye mwenyewe.

Akizungumza na Showbiz-Xtra, Nay alisema kuna baadhi ya mashabiki hata uwaambie nini huwa hawawezi kukuelewa hivyo kwa sasa kila atakayemuuliza kuhusu uhusiano wake na Nini, atakuwa hana jibu zaidi ya kusema ukweli anao moyoni.

 

“Unajua ukiwaambia watu kwamba ni rafiki tu, hawakuelewi. Ukiwaambia kwamba mnafanya naye tu kazi hawakuelewi basi mimi nafikiri kwa sasa itoshe tu kusema kwamba jibu ninalo moyoni mwangu,” alisema Nay.

Nay na mrembo Nini wamekuwa wakihusishwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi hususan baada ya kufanya kazi pamoja katika Wimbo wa Niwe Dawa wa mrembo huyo.

SHOWBIZ-XTRA

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment