The House of Favourite Newspapers

NBAA Yatoa Milioni 15, Hospitali Ya Muhimbili Kwaajili Ya Watoto Wanaogua Saratani

0
Mkurugenzi wa NBAA, CPA Pius Maneno

Dar-es-Salaam, 30 Novemba 2023: Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo Upanga Dar, Dk. Julieth Magandi amepokea cheki ya shilingi milioni 15, kutoka Bodi ya Uhasibu nchini (NBAA) kwa ajili ya kusaidia watoto wanaugua ugonjwa wa saratani.

Akizungumza  wakati wa kutoa shukrani kwa NBAA, Dk. Julieth Magandi, amesema kiasi hicho pesa ni msaada mkubwa sana kwao kwakuwa ukizingatia wanapokea watoto kutoka ndani na nje ya nchi na wenye changamoto za kifedha za kuweza kumudu gharama za matibabu.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo Upanga Dar, Dk. Julieth Magandi.

Amesema wanatoa msamaha kwa wagonjwa ambao wanachangamoto ya kumudu gharama za matibabu kwa sababu ni kubwa, kuanzia kwenye vipimo, matibabu hadi madawa wengi hushindwa gharama hizo hivyo pesa hizi zitaenda kuwasaidia.

“Kwa mwaka tunatoa msamaha wa matibabu bilioni 1.7 na ukichukulia kati ya hiyo misamaha yote karibu asilimia 9 mpaka 10 ni kwa ajili ya watoto wadogo wenye saratani. “Hii sana sana inahusisha malazi, madawa, vipimo vya maabara na dialojia hivyo, basi nichukue nafasi hii kuwashukuru kwa kuja na wazo hili la kutusaidia.” Amesema.

Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wadau wengine kujitokeza na  wasichoke kuwasaidia watoto na watu wengine wenye changamoto mbalimbali za matibabu.

Mkurugenzi wa NBAA, CPA Pius Maneno akimkabidhi mfano wa hundi Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Julieth Magandi.

Nae Mkurugenzi wa NBAA, CPA Pius Maneno amesema kuwa huwa kila mwaka wanakuwa na mkutano mkuu hivyo mwaka huu wameona wafanye matendo ya huruma na moyo wa kizalendo kwa kuwakumbuka watoto wanauguzwa saratani hospitalini hapo.

“Tunashukuru kwa kasi aliyonayo Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambayo inatupa nguvu ya kuweza kufanya kazi kwa bidii hivyo tumekuja hapa kurejesha furaha kwa watoto hawa kwa kuchangia kiasi hicho Cha fedha kwa ajili ya huduma kwa watoto hawa wanaogua Saratani”, amesema Bw. Maneno.

Mambo ya Jogging yalivyokuwa Bagamoyo.

Amewapongeza wafanyakazi wenzake kwa kufanya kazi kwa bidii na wataendelea kuchangia huduma za kijamii. Sambamba na kufika hospitalini hapo walianzia na mbio za kujifurahisha za kilometa 5 na 10 pamoja na mashindano ya kuogelea Bagamoyo.

Mbio hizo zimehusisha utoaji wa zawadi mbalimbali kwa washindi wa kwanza mpaka wa tatu wa michezo hiyo.

Mkurugenzi wa Huduma za Viwango vya Kiuhasibu, Utafiti na Huduma za Ufundi wa NBAA, Angyelile Tende.

Akizungumza baada ya  michezo hiyo, Mkurugenzi wa Huduma za Viwango vya Kiuhasibu, Utafiti na Huduma za Ufundi wa NBAA, Angyelile Tende, amesema lengo la kuendesha michezo hiyo ni kuhamasisha washiriki kuchangia kiasi cha fedha milioni 15 kwa ajili ya kwenda kuwasaidia watoto wanaougua magonjwa ya saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Wadau wakishuhudia tukio la kukabidhi hundi hiyo.

Amesema washiriki waliojitokeza katika michezo hiyo ni 800 na kwamba lengo lao limekamilika kama walivyopanga. Kongamano hilo la Bodi ya Wahasibu linatarajiwa kufungwa kesho Ijumaa.

Leave A Reply