The House of Favourite Newspapers

NCCR Yaungana na Chadema Kususia Mkutano

0

VYAMA vya NCCR-Mageuzi na Chadema vimeungana kususia mkutano ulioitishwa na Baraza la Vyama vya Siasa. Mkutano huo wenye la lengo la kuondoa mvutano kati ya vyama vya siasa na jeshi la polisi utafanyika Desemba 16 na 17, Dodoma huku Rais Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kuwa mgeni rasmi pamoja na wadau mbalimbali wa siasa.

 

Hiyo ni mara ya pili kwa vyama hivyo kususia vikao vinavyoitishwa na baraza hilo baada ya jana Chadema kutoa muelekeo kama huo kwa madai kwamba sababu zilizowafanya wasishiriki mkutano uliopangwa kufanyika Oktoba 21 na 22 ambao baadae ulihailishwa hazijafanyiwa kazi ikiwamo kunyimwa uhuru wa kikatiba wa kutekeleza majukumu yao ya kisiasa.

 

Hata hivyo Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa hilo,Juma All Khatibu ameviomba vyama hivyo kulegeza misimamo yao kukubali kushiriki na kuelewa changamoto wanapima.

 

Akizungumza Dar es Salaam Leo Desemba 13-2021,Naibu Katibu Mkuu Bara wa chama hicho Cha NCCR-Mageuzi,Anthony Komu amesema kulingana na ratiba waliyopewa hawaoni kama kikao hicho kinaweza kutoa majibu kwa kile wanachokilalamikia.

 

“Tulitoa msimamo kwenye kikao cha kwanza ambacho baadae kiliahirishwa bado tunaendeleza kwa sababu hatujaona mabadiliko na hiki kikao kinachoenda kufanyika muongozo tulioletewa hauoneshi kama tutapata nafasi ya kueleza malalamiko yetu,” amesema Komu.

 

Amesema wataanza kushiriki vikao hivyo hadi pale Rais Samia atakapokubali kuonanao na kueleza malalamiko yao kwa kile wanachokiona.

 

“Nawaomba walegeze msimamo wajekushiriki kwakuwa kikao hiki kitahusisha wadau wengi wa siasa ikiwamo Serikali ambapo watapata nafasiya kueleza kile wanachokilalamikia na kutafutiwa ufumbuzi,”Amesema Khatibu

Leave A Reply