The House of Favourite Newspapers

NCHI ZENYE WATU WANAOISHI UMRI MKUBWA ZAIDI DUNIANI

Tokeo la picha la OLD PEOPLE

JUKWAA la Uchumi Duniani (WEF) limetoa utafiti wa nchi ambazo watu wake wanaishi umri mkubwa zaidi.  Utafiti huo haukutia maanani tu nguvu ya kifedha ya nchi husika bali afya ya watu katika nchi hizo.

Utafiti huo umelinganishwa dhidi ya takwimu za nchi za umoja wa ushirikiano wa maendeleo ya kiuchumi  (OECD) kujua ni kwa nini watu huishi umri huo mrefu.

Nchi hizo na nafasi zake, umri na sababu zake ni:

13. Sweden — miaka 82.  Sababu kuu ni maji safi.

12. Iceland — 82.1. Chakula bora kinachopunguza hatari ya magonjwa ya kisukari na moyo.

11. Jamhuri ya Korea (Kusini) — 82.2 kustawi kwa uchumi na kuboreshwa kwa maisha licha ya kiwango cha uchafuzi wa mazingira kuwa juu.

10. Luxembourg — 82.2. Idadi ndogo ya watu na kipato cha juu, mambo yanayowapa chakula bora na matibabu bora.

9. Israel — 82.2. Wanaume ndiyo huishi umri mrefu zaidi licha ya kulazimika kulitumikia jeshi.

8. Australia — 82.3. Huduma nzuri ya afya.

7. France — 82.4. Idadi ndogo ya watu wenye vitambi.

6. Singapore — 82.6. Matibabu mema na kinga za magonjwa.

5. Italy — 82.7. Tiba njema, kipato kikubwa kinachowawezesha kula na kuishi maisha mazuri.

4. Switzerland — 82.8.  Tiba na chakula bora.

3. Spain — 83.1. Chakula bora hasa mboga, samaki na vyakula vya mafuta..

2. Japan — 83.6. Chakula bora.

1. Hong Kong — 84. Chakula bora chenye kukaushwa na unywaji wa chai.

Comments are closed.