The House of Favourite Newspapers

‘NDEGE YA WACHAWI’ YAANGUKA NEWALA – VIDEO

Chombo kinachodaiwa kuwa ni ‘Ndege ya Wachawi’ kimeanguka katikati ya barabara wilayani Newala Mkoani Mtwara na kuzua taharuki miongoni mwa wakazi wa eneo hilo.

Tukio hilo la aina yake limejiri hivi karibuni wakati chombo hicho maarufu kwa jina la ‘ungo’ kilipodondoka wakati kikikatiza angani.

Kwa mujibu wa mshuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa, kuanguka kwa ‘ndege ya wachawi’ yawezekana kilipita kwenye njia isiyo sahihi na kupoteza mwelekeo au kiliishiwa mafuta, japo ilikuwa vigumu kuthibitishwa kama kweli ni chombo cha wachawi au ni kitu kingine.

Popote ulipo unapokutana na tukio ambalo unaweza kulinasa kwa njia ya video ya simu yako, basi usisite kufanya hivyo na kisha tutimie kwa WhatsApp 0753 715 779 (+255753715779). Tunalipa vizuri video za habari na matukio ya kwanza kutufikia.

TAZAMA VIDEO: ‘NDEGE YA WACHAWI’ YAANGUKA NEWALA 

 

Comments are closed.