The House of Favourite Newspapers

Exclusive: Ndoa ya Kanye West na Kim Kardashian Chali

kim-na-kanye-1 Umeinyaka hii au kuisikia popote pale? Ile ndoa ya masupastaa iliyofungwa mwaka 2014 kati ya mwanamuziki, Kanye West na Kim Kardashian ambayo ilikuwa gumzo kila kona, hatimaye ubuyu kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari vya kidaku nchini Marekani na watu wa karibu unasema kwamba ndoa hiyo imevunjika.

kim-na-kanye-3Siku chache kabla ya kuvunjika kwa ndoa hiyo iliyojawa misukosuko ya usaliti na maumivu ya mapenzi zinasema kuwa chanzo kikubwa cha ndoa hiyo kuvunjika ni ile video ambayo ilinaswa ikimuonyesha Kanye akifanya mapenzi na mwanamke mmoja kipindi cha nyuma wakati tayari alikuwa kwenye ndoa na Kim.

kim-na-kanye-2“Imevunjika,” ni neno pekee ambalo limekuwa likitamkwa na watu wa karibu na kitu kilichoupa nguvu ubuyu huyo ni kwamba kwa mara ya kwanza, Kim ameonekana akitanua mitaani pasipo kuwa na pete kidoleni,  kitu kinachoupa nguvu ubuyu huo.

kim-na-kanye-4

Nay wa Mitego Ametoboa Siri: Hiki ndicho Alichokimiss kwa Shamsa Ford

Comments are closed.