The House of Favourite Newspapers

Ndoa ya Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho Yatikisa Dar (Video)

0
Meneja Abdallah Mrisho na mkewe, Catherine Mdami wakiwa katika pozi la furaha, muda mfupi baada ya kufungwa kwa ndoa yao.
Meneja Mrisho na mkewe, wakiwa na wapambe wao (walioshika magazeti), wakifurahi kwa pamoja baada ya kufungwa kwa ndoa yao, Jumamosi, Septemba 30, 2017 jijini Dar es salaam.
Bibi Harusi, Catherine (katikati) akiwa amezungukwa na wapambe wake.
Daaab! Bwana na Bibi Harusi wakiwa wamezungukwa na wapambe wao wakiwa katika pozi maarufu kwa jina la dab!
Maharusi wakiwa na wasimamizi wa ndoa yao, Bi Justina Mberesero (Matron) na Said Mdoe (Best Man).
Wakifurahia jambo kwa pamoja mara baada ya kufungwa kwa ndoa yao.

Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, jana (Jumamosi, Sept. 30,2017) alifunga ndoa ya kifahari na Catherine Mdami, iliyolifanya Jiji la Dar es Salaam lisimame kwa muda kutokana na maandalizi yake bab’kubwa, ikifuatiwa na sherehe ya kukata na shoka iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City.

Katika sherehe hiyo ambayo MC alikuwa ni mtangazaji wa Clouds TV, Harris Kapiga, wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers wakiongozwa na mkurugenzi wao, Eric Shigongo, ndugu, jamaa na marafiki, walijumuika kula, kunywa mpaka kusaza na kucheza muziki mzuri, mpaka usiku sana huku kukiwa na ‘special appearance’ ya Mbunge wa Mtama, Mhe. Nape Nnauye na msanii wa Bongo Movie, Jackline Wolper.

Kwa upande wa burudani, Bendi ya Banana Zorro (B-Band), ikiongozwa na Banana mwenyewe pamoja na msanii wa kitambo kwenye muziki wa kizazi kipya, Nuruely, iliangusha burudani ya nguvu, ikipiga ‘cover’ ya nyimbo mbalimbali zilizowaburudisha vilivyo waliohudhuria.

Harusi ya Abdallah na Catherine, Mlimani City – Part 1

Harusi ya Meneja Abdallah na Catherine, Mlimani City – Part 2

Leave A Reply