The House of Favourite Newspapers

Ndoa ya Mpoto yatikisika

0

HAKUNA kisa zaidi ya madai kwamba yeye ni memba wa Freemason, ndoa ya nyota wa nyimbo za mashairi Bongo, Mrisho Mpoto imetikisika, Amani limejua.

Kwa mujibu wa chanzo, baada ya habari na picha zake kutoka  kwenye gazeti hili wiki mbili zilizopita, ndugu wa Mpoto walikuja juu wakisema kuwa, kwa kitendo cha staa huyo kuingia kwenye imani hiyo ni hatari kwa mkewe, Mariam na watoto wawili.

“Ndugu wanaamini Freemason wanachukua watu makafara. Walipoona Mpoto kanaswa akitokea kwenye Jengo la Freemason (Posta, Dar) wakajua sasa mtoto wao anaweza kutolewa kafara siku yoyote.

“Mpoto aliwaalika kwenye Sikukuu ya Iddw El Haji wakagoma kushiriki. Lakini majirani wa nyumbani kwa Mpoto, Mbagala, Dar nao wameanza kumkwepa, si kama zamani,” kilisema chanzo.

Baada ya madai hayo, Amani lilimvutia waya Mpoto kwa lengo la kuweka sawa mizani ya habari ambapo alisema:

“We ndugu yangu acha tu. Ukweni ni moto. Wanajua mimi Freemason. Nimewaeleza lakini wapi! Mke wangu yeye kidogo kaelewa, lakini anauliza je ikitokea akafa ghafla, si nduguze watasema nimemchukua kafara?”

Katika toleo la gazeti hilo, ukurasa wa 16 kulikuwa na habari yenye kichwa; marafiki wadai…MPOTO NI FREEMASON.

Katika habari hiyo, vyanzo vilimwona msanii huyo akiwa kwenye Jengo la Freemason hivyo kuliambia Amani. Mapaparazi walipofika walimnasa kwa picha na baadaye walipomuuliza, Mpoto alijitetea kuwa alifika pale kuonana na mgombea ubunge mmoja ambaye alitaka kumtungia mashairi.

 

 

Leave A Reply