The House of Favourite Newspapers

Ndoa ya Zari na GK Choppa Yanukia

0

SIYO stori kwamba ‘baby mama’ wa staa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady yupo kwenye penzi jipya na kijana ‘barobaro’ aitwaye GK Choppa.

 

Zari na Choppa; wote ni raia wa nchini Uganda wenye maskani yao Durban nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uganda vilivyozungumza na wawili hao, huenda Zari na Choppa tayari wanaishi pamoja nyumbani kwa mwanamama huyo mwenye watoto watano.


Vyombo hivyo vya habari za burudani vinaeleza kwamba, Choppa ameanza mipango ya ndoa akianza na pete ya uchumba ambayo tayari amemvalisha Zari na kinachofuata sasa ni ndoa.

 

“Yes, I’m going to make it official (Ndiyo, nakwenda kufanya iwe rasmi),” anasema Choppa katika video na kuongeza; “Nakwenda kumvalisha pete ya ndoa kwa sababu sipendi kuona mtu akimkosea heshima. Mimi ndiye mwanaume wake wa mwisho.”

Kwa upande wake, Zari alipokuwa akiruka live kunako Insta Live anakiri kupata mwanaume mpya hivyo hataki kuulizwa kuhusu watu wengine akimaanisha Diamond.

 

Zari amekuwa akionekana kwenye video mbalimbali zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii na mwanaume huyo akimhudumia na kumpetipeti kiasi cha kusifiwa kuwa anajua kumtunza mwanaume wake.

Leave A Reply