The House of Favourite Newspapers

Ndoa za Mastaa Zinazoshamiri Licha ya Tofauti za Umri

1 . Sylvester Stallone na Jennifer Flavin
Tofauti ya umri kati yao ni miaka 22.
Wawili hawa walikutana mwaka 1988 wakati mume alikuwa na umri wa miaka 42 na mke alikuwa na miaka 20.  Walioana mwaka 1997, na japokuwa walikuwa wanatengana mara kwa mara, walirudiana na hadi sasa wako pamoja ambapo wamezaa  watoto wa kike: Sofia (aliyezaliwa 1996), Sistine (1998) na Scarlet (2002).

2. Warren Beatty na Annette Bening
Tofauti ya umri miaka 21
Waigizaji hao walikutana mwaka 1990 na kuoana miaka miwili baadaye na hadi sasa wana watoto wanne: Stephen (1992), Benjamin (1994), Isabel (1997) na Ella (2000).

3. Harrison Ford na Calista Flockhart
Tofauti miaka 22
Han Solo alikutana na  Flockhart  mwigizaji mwanzake 2002 na kuoana ambapo hadi leo wako pamoja wakiwa na mtoto wa kuasili aitwaye Liam aliyezaliwa 2001.

4. Pierce Brosnan na Keely Shaye Smith
Age Gap: 10 years
Mwigizaji Brosnan na mwandishi wa habari, Smith, walikutana 1994 huko Mexico na kufunga ndoa miaka saba baadaye na bado wako pamoja wakiwa na watoto wawili: Dylan Thomas (1997) na Paris Becket (2001). Kabla ya kumwoa Smith, Brosnan alikuwa amemwoa mwigizaji Cassandra Harris, aliyekufa kwa kansa ya kizazi mwaka 1991.

5. Jay-Z na  Beyoncé
Tofauti ya umri miaka 12
Wanamuziki hao maarufu duniani, walianza kuwasiliana mwaka 2002 wakati Jay-Z akiwa na miaka 33 na Bey akiwa na miaka 21 na wakafunga ndoa 2008 ambapo wanaendelea kuwa pamoja wakiwa wazazi wa Blue Ivy Carter (2012) and mapacha Sir na  Rumi Carter (2017).

6. Kevin Costner na Christine Baumgartner
Tofauti miaka 19
Mwigizaji Costner alikutana na mwanamitindo  Baumgartner mwaka  2000 wakafunga ndoa miaka minne baadaye.  Wakiwa bado pamoja hadi leo wamezaa watoto watatu: wawili wa kiume Cayden (2007), Hayes (2009) na binti Grace (2010).

7. Derek na Hannah Jeter
Tofauti miaka16
Mastaa hao waigizaji walioana mwaka 2016 huko California na wanaendelea kuwa pamoja wakiwa na binti aitwaye  Bella Raine aliyezaliwa 2017.

 

 

 

 

 

Comments are closed.