The House of Favourite Newspapers

Breaking: Moto Wazuka Jengo la Benjamin Mkapa – Video

Moto umezuka leo katika jengo la Benjamin Mkapa, Millennium Tower – Dar ambapo unasadikiwa umeanzia kwenye ghorofa ya tatu. Wageni na wafanyakazi wamekimbia kwa taharuki huku ikidikiwa kuna wengine wamekwama kwenye lifti ya jengo hilo.

Mkaguzi msaidizi wa kikosi cha zimamoto na uokoaji, Elinimo Shang’a amesema chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme ilioanzia stoo na kwamba kutokana na uwazi katika chumba hicho, moshi ulisambaa na kusababisha taharuki.

Kuhusu madhara amesema hakuna madhara kwa mtu yeyote lakini uchunguzi unaendelea kujua hasara iliyopatikana.

Endelea kufuatilia taarifa zetu kupitia Global Habari Updates, tutakujuza.

Comments are closed.