The House of Favourite Newspapers

Ndugai Apangua Safu ya Wajumbe Kamati za Kudumu za Bunge

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amefanya uteuzi mpya wa wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge ambapo amesema amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa Ibara ya 96 ya Katibu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

“Kanuni ya 116(1) inaweka utaratibu kwamba, ujumbe kwenye Kamati za Kudumu za Bunge utadumu mpaka mwisho wa Mkutano wa Kumi wa Bunge ambao ni nusu ya kwanza ya maisha ya Bunge.

 

“Kwa mamlaka niliyopewa na Kanuni ya 115(3) na kwa kuzingatia vigezo vilivyoanishwa katika Kanuni ya 116(5) nimefanya uteuzi mpya wa ujumbe katika Kamati za Kudumu za Bunge. Wajumbe wa kila kamati wanawajibika kuchagua mwenyekiti na makamu mwenyekiti kwa mujibu wa Kanuni ya 116(10) kuwa viongozi wao,” anasema Spika Ndugai.

Orodha ya Majina ya Wajumbe wa Kamati Za Bunge

Comments are closed.