The House of Favourite Newspapers

Ndugai Kuwashtaki Mawaziri Watoro Kwa Rais Magufuli

magufuli-na-ndugai

Rais John Pombe Magufuli akiwa na Spika wa Bunge Job Ndugai (picha na maktaba)

DODOMA Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema ana orodha ya wabunge na mawaziri waliokithiri kwa utoro bungeni, hivyo kuwataka kubadilika huku akitishia kuwaanika na kuwashitaki hadi kwa Rais John Magufuli.

Alisisitiza kutotania katika suala hilo na kuongeza kuwa mahudhurio katika Mkutano wa Tano wa Bunge la 11 unaotarajiwa kuanza Novemba mosi mwaka huu, ndiyo utakaokuwa kipimo chao cha mwisho.

Aliyasema hayo bungeni jana muda mfupi baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuahirisha vikao vya Mkutano wa Nne wa Bunge hilo lililokutana kwa wiki mbili kuanzia Septemba 6, mwaka huu.

“Kuna orodha nimeiandaa ya watoro katika kamati, lakini kwa leo sitawataja hapa kwa sababu nimeona tuendelee kuwafuatilia katika vikao vijavyo. Kama hawatabadilika nitawaambia waajiri wao, yaani wabunge watoro nitawasema kwa wananchi wao na kwa viongozi wa vyama vyao na kwa mawaziri watoro, nitamwambia namba moja, kwamba mawaziri hawa hawawajibiki ipasavyo.” Alisisitiza.

 

Comments are closed.