The House of Favourite Newspapers

NECTA Yatangaza Matokeo ya Darasa la Nne, Kidato cha Pili, Ufaulu Washuka

0

 

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya upimaji wa kitaifa wa darasa la nne na kidato cha pili kwa wanafunzi waliofanya mtihani mwaka 2022.

Akitangaza matokeo hayo Kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA, Athumani Amasi amesema ufaulu umeshuka ikilinganishwa na mwaka 2021 ambapo kwa darasa la nne ufaulu ni asilimia 82.95 ikilinganishwa na asilimia 86.30 mwaka 2021.

Kwa upande wa kidato cha pili ufaulu ni asilimia 85.18 ikilinganishwa na mwaka 2021 ambapo ufaulu ulikuwa asilimia 92.32.

Aidha, NECTA imezuia matokeo ya wanafunzi 442 wa darasa la nne na wanafunzi 258 wa kidato cha pili waliopata matatizo ya afya na kushindwa kukamilisha mtihani wa upimaji wa kitaifa.

Pia, imefuta matokeo ya wanafunzi 213 wa darasa la nne na wanafunzi 52 wa kidato cha pili ambao walibainika kufanya udanganyifu.

Wakati huo huo, NECTA imefungia vituo viwili kati ya vituo 18,645 vya mitihani vilivyothibitika kupanga na kufanya udanganyifu.

 

BOFYA KUTAZAMA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI: Matokeo ya Kidato cha Pili

 

BOFYA KUTAZAMA MATOKEO YA DARASA LA NNE: Matokeo ya Darasa la Nne

 

Leave A Reply