The House of Favourite Newspapers

Nelly, Jux Kitu na Boksi?

0

 KITU na boksi! Ndiyo maneno unayoweza kusema kutokana na mrembo ambaye amewahi kutwaa mataji kibao ya urembo Bongo, Nelly Kamwelu kusema kuwa yeye na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Juma Jux ni marafiki wazuri sana.

 

Akizungumza na Wikienda, Nelly alisema watu wengi wanamuuliza kuhusiana na Jux kwani video za nyimbo zake nyingi anamtumia kama video queen au kuna mahusiano ya kimapenzi baina yao.

 

“Nashangaa watu wakiona nacheza video za Jux wanasema kuna kitu kinaendelea baina yangu na yeye, kumbe hakuna kitu chochote, ukweli ni kwamba sisi ni marafiki wazuri sana tangu zamani na tunapendana sana,” alisema Nelly.

STORI: IMELDA MTEMA

Leave A Reply