The House of Favourite Newspapers

Nelly; Nimesoma magazeti ya Global kwa miaka 18

0

nellys Nelly Mwangosi na mumewe.

NA FRANCIS GODWIN, IRINGA

NELLY Mwangosi, mwanamama mwenye umri wa miaka 45, mkazi wa Kibwabwa Kata ya Kitwiru mkoani Iringa ni mshindi wa Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba, iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam wiki iliyopita na Kampuni ya Global Publishers, inayochapisha magazeti pendwa na michezo Tanzania.

nellys2Nelly Mwangosi nafamilia yake.

Katika kile alichodai kutoamini macho na masikio yake, Nelly ambaye ni mama wa nyumbani, mke wa Mwalimu wa Chuo Cha Ufundi Stadi (VETA), Karolo Stephen Magani (52), anasema kwa miaka 18, amekuwa akisoma Magazeti Pendwa ya Global Publishers, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda na kitu cha ajabu, katika muda wote huo hakuwahi kushiriki shindano lolote, licha ya kuwa yametokea mengi.

“Mimi na familia yangu ni wapenzi wakubwa wa magazeti ya Global kwa sababu ya aina za habari zake ambazo ni za uhakika, mume wangu yeye ni msomaji wa Gazeti la Championi na huwa hakosi kununua kila wiki mara mbili,” anasema Nelly.

nellys1“Katika awamu hii ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba sikuacha kununua gazeti na kukata kuponi na kutuma. Mume wangu alikuwa akitembea umbali wa zaidi ya Km 5 kwenda mjini eneo la Posta kwa muuza magazeti, Mashaka Kayoka kununua na kukata kuponi na kuituma,” anasimulia mama huyo.

Bi. Nelly ambaye hakuwahi kuwaza kuwa na nyumba jijini Dar es Salaam, amesema baada ya kukabidhiwa mjengo huo, atakaa na mumewe ili kufikia uamuzi wa sehemu ya kuishi, kati ya Iringa na Dar es Salaam kwani siku zote amekuwa akitamani kuishi katika jiji hilo.

Licha ya kuwa mama wa nyumbani, Nelly pia amekuwa akijishughulisha na ujasiriamali na ni mfuatiliaji mzuri wa elimu ya ujasiriamali inayotolewa na Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo, ambayo amekuwa akitoa kupitia semina mbalimbali.

Nelly amewaasa wasomaji waliokuwa hawaamini kama bahati nasibu zinazochezeshwa na Global ni za ukweli waondokane na mtazamo huo kwani ushuhuda wa jambo hilo umemtokea yeye.

“Wakati nanunua magazeti ya Global, kujaza kuponi na kuzituma kuna jirani yangu alikuwa akinitania kwamba nilikuwa napoteza muda kwani nyumba hiyo ilikuwa imeandaliwa kwa mtu f’lani, lakini baada ya kutangazwa mshindi ameamini na ameahidi ataanza kuyasoma magazeti hayo,” alisema Nelly.

Leave A Reply