testiingg
The House of Favourite Newspapers

Neymar Afunguka Anavyofurahia Penzi la Mpenzi Wake Mpya Bruna Biancardi

0

SUPASTAA wa soka, Mbrazili, Neymar Jr, amefunguka jinsi anavyompenda mpenzi wake mpya, Bruna Biancardi, walipokuwa wakisherehekea bethdei ya mrembo huyo kutimiza miaka 28 juzi.

 

Neymar, 30, aliandika: “Bruh, mzuri. Nakutakia mema yote katika dunia hii, nakuombea utimize malengo yako yote. Siku ni yako lakini zawadi ni yetu. Kwa hiyo nina furaha kuwa nawe maishani mwangu. Nakupenda.”

 

Awali, Bruna alimshukuru Neymar kwa kuipa umaalum bethdei yake. “Nakupenda,” aliandika Bruna.

RIO DE JANEIRO, Brazil

Leave A Reply