The House of Favourite Newspapers

Neymar Kufanyiwa Upasiuaji, Kukaa Nje Miezi Miwili, World Cup Vipi?

IKIWA imesalia miezi mitatu tu ili Brazil icheze mchezo wake wa Ufunguzi wa Kombe la Dunia dhidi ya Switzerland nchini Urusi, timu ya Madaktari ya PSG na timu ya Taifa ya Brazil kukutana, wamefikia uamuzi wa kumfanyia upasuaji wa kifundo cha mguu mshambuliaji Neymar JR aliyeumia mwisho wa juma lililopita wakati wa mchezo wao na Marseille.

 

Zoezi hilo litafanyika mwisho wa wiki hii nchini Brazil, anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili ambapo atauoksa mchezo wa marudiano na Real Madrid Kombe la Vilabu Bingwa Ulaya.

 

Neymar alijiunga na PSG mwezi Agosti mwaka jana akitokea Barcelona ambapo usajili wake ulivunja rekodi baada ya kugharimu kiasi cha pauni milioni 200. Mpaka sasa ameifungia mabao 29 kwenye mechi 30 alizocheza.

Comments are closed.