The House of Favourite Newspapers

Ngoma Mpya ya Diamond na Ne-Yo Kutamba Kwenye TV na Redio za Marekani


diamond-platnumz-na-neyo-marry-meSTAA wa Bongo fleva asiyekuwa na mpinzani Afrika Mashariki, Diamond Platnumz amesema kwamba wimbo wake mpya ambao haujatoka ‘Marry You’ aliomshirikisha staa kutoka Marekani, Ne-Yo utachezwa hadi kwenye vituo vya redio na runinga vya nchini Marekani.

Mkali huyo wa ngoma ya ‘Salome’ amesema kuwa nyimbo nyingi za wasanii wa Afrika walizowashirikisha wasanii wa Marekani zimekuwa hazichezwi nchini humo.

diamondAkifanya mahojiano na Kipindi cha 255 kinachorushwa na cha Clouds FM, Diamond ameeleza haya.

“Namshukuru Mungu Ne-Yo kanitunuku ni kama bahati wimbo wangu uchezwe mpaka Marekani lakini kwa wasanii wengine wanakataaga,” alisema. 

Mpaka sasa tayari video ya wimbo huo imeshafanyika na kukamilika tangu mwezi Septemba mwaka huu jijini Los Angeles, Marekani lakini licha ya kwamba haijajulikana muda wa kuachiwa rasmi.

Comments are closed.